Haruna
Niyonzima amekuwa gumzo kwenye Simba Day kutokana na namna ambavyo
amesajiliwa lakini kubwa akiwa ametoka kwa watani wao wa jadi Yanga
,ambapo amekuwa mmoja ya wachezaji ambao leo ameichezea klabu yake ya
Simba dhidi ya Rayon Sport kutoka Rwanda huku mchezo ukimalizika kwa
Simba kupata ushindi wa goli 1-0.
Lengo
kubwa la mchezo huo lilikuwa ni kutambulisha kikosi cha Simba
kitakachocheza mashindano mbalimbali msimu ujao. Imekuwa desturi kwa
Simba kutambulisha wachezaji wao siku ya August 8 kila mwaka huku
siku hiyo ikijulikana kwa Simba Day.
Goli
pekee la mchezo huo limefungwa na kiungo mshambuliaji Mohamed Ibrahim
dakika ya 16 kipindi cha kwanza akiwa amepokea pasu kutoka kwa
Emanuel Okwi na bao hilo kudumu kwa dakika zote za mchezo.
Miongoni
mwa wachezaji wapya waliotambulishwa ni Aishi Manula, Said Mohamed
‘Nduda’, Erasto Nyoni, John Bocco, Paul Mukaba, Ally Shomari,
Yusuph Mlipili na Salim Mbonde
Wengine
ni Nicolas Gyan, Shomari Kapombe Emanuel Okwi na Haruna Niyonzima.
No comments:
Post a Comment