Mchezo wa fainali ya Super Cup
kati ya mabingwa wa Champions league Real Madrid dhidi ya mabingwa wa
Europa League klabu ya Manchester United.
Mchezo huo uliopigwa Telekom Arena
ulikuwa unasubiriwa sana na mashabiki wa soka kutokana na ushindani
baina ya vigogo hawa wakubwa wa soka duniani.Real Madrid walianza
kulichungulia lango la Manchester United dakika ya 24 kupitia kwa
Casemiro ambapo bao hilo lilidumu kwa kipindi chote cha kwanza.
Kipindi cha pili Real Madrid
walioonekana kuliandama sana lango la Manchester United walipata bao
la pili dakika ya 52 na safari hii alikuwa ni Isco aliyeitungua
United.Romelu Lukaku amedhihirisha kwamba amekuja Manchester United
kwa kazi moja tu ya kufunga kwani katika dakika ya 62 aliipatia
United bao la kufutia machozi.
No comments:
Post a Comment