Michuano
ya Ndondo Cup 2017 imemalizika leo Agosti 13, 2017 kwa mchezo wa
fainali kati ya Goms United dhidi ya Misosi FC mechi iliyochezwa
kwenye uwanja wa Kinesi,Misosi FC wameibuka mabingwa wapya wa Ndondo
baada kuifunga Goms kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya kufungana
1-1 katika dakika 90 za kawaida.
Mechi
hiyo ya fainali imeshuhudiwa na Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Mh. Tulia Ackson, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
Paul Makonda, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi, Mbunge wa Mtama
Nape Nnauye na wadau mbalimbali wa soka.
Misosi
wameichapa Goms kwa jumla ya penati 5-4 na kubeba kombe hilo la
Ndondo ikiwa ni mara yao ya kwanza, Misosi wamepata kitita cha
shilingi milioni 10 kwa kuwa mabingwa wa Ndondo Cup huku Goms
wakijinyakulia shilingi milioni tano baada ya kuwa washindi wa pili
wa mashindano
No comments:
Post a Comment