Cosafa Cup imeendelea Julai 5,
2017 ambapo Taifa Stars ya Tanzania imekutana na timu ya Taifa ya
Zambia kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano ya mwaka huu.
Taifa Stars imeshindwa kusonga
mbele kwenye mashindano ya Cosafa baada ya kupoteza mchezo kwa
kufungwa 4-2 na kuiacha Zambia ikisonga mbele kucheza fainali ya
michuano hiyo nchini Afrika Kusini.
Magoli ya Stars yamefungwa na
Erasto Nyoni dakika ya 14 ambaye alifunga goli la kwanza kisha Simon
Msuva akafunga goli la pili dakika ya 85 wakati magoli ya Zambia
yakifungwa na Mwila dakika ya 44 kisha Shonga akafunga dakika ya 45+2
Zambia wakapata goli la tatu kwa mkwaju wa penati uliofungwa na
Chirwa dakika ya 56 halafu Shonga akafunga bao la nne likiwa ni goli
lake la pili dakika ya 68.
No comments:
Post a Comment