Rais
Kenyatta ameahidi kuwa serikali yake itaunda nafasi mpya za kazi
Milioni 6.5 kwa muda wa miaka mitano atakayokuwa madarakani. Ameeleza
kuwa hili litafanyika kwa kuhakikisha kuwa anajenga kiwanda kimoja
katika Kaunti zote 47 nchini humo.
Elimu
katika Shule za serikali za Sekondari itakuwa bure. Hakuna mwanafunzi
yeyote atakayelipa ada ili kupata elimu,Kenyatta ameahidi kuimarisha
sekta ya afya nchini humo kwa kupanua hospitali, kununua vifaa na
kuinua kiwango cha tiba katika hospitali za serikali nchini humo.
Wanawake
waja wazito nchini humo wataendelea kujifungua bure na kupata huduma
muhimu bila malipo yoyote nchini humo kwa mujibu wa Ilani ya
Jubilee,Kiongozi huyo wa Jubilee ameahidi ikiwa atashinda atajenga
makazi ya bei nafuu 500,000 nchi nzima lakini pia mabwawa ya maji 57
kwa lengo la kuimarisha sekta ya kilimo nchini humo.
Pamoja
hayo, Kenyatta amesema ikiwa atachaguliwa tena Wakenya wote
wataunganishwa na nguvu za umeme kwa muda wa miaka mitatu ya uongozi
wake.Ahadi nyingine iliyotolewa na kiongozi huyu ni kujenga viwanja
vipya vya kisasa vya michezo katika maeneo mbalimbali nchini
humo.Kenyatta amesema serikali yake inaimarisha usalama, kujenga reli
ya kisasa lakini pia kuinua uchumi wa taifa hilo.
No comments:
Post a Comment