Mshindi
mara nane wa michuano ya Olimpiki Usain Bolt amesema anaweza
kuendelea kukimbia hata baada ya mbio za dunia mwaka 2017 lakini
itakuwa mara yake ya mwisho kufanya hivyo.
Bolt
raia wa Jamaica mwenye miaka 30, awali alisema kuwa mbio zake za
mwisho zingelikuwa za London mwezi Agosti.Akiongea siku ya Jumatatu
Bolt amesema amefanya mazungumzo na kocha wake Glen Mills na
kuafikiana juu ya kuhitimisha safari yake mwakani.
Bolt
amekuwa mmoja wa wakimbiaji mashuhuri duniani huku akitajwa kama
binadamu mwenye kasi zaidi.
No comments:
Post a Comment