Leo june
27 2017,Taifa Stars Baada ya kuwagalagaza Malawi kwenye mchezo wa
kwanza kwenye michuano ya Cosafa Castle Cup,sasa Stars watashuka
dimbani kuchuana na Angola.
Mchezo
huo unatarajiwa kufanyika pale kwenye uwnja wa “Royal Bafokeng
Sports Palace” huku Timu zote mbili zikiwa na pointi sawa mkononi
kwa kumiliki pointi 3 kila timu lakini Taifa star wakiwazidi Angola
kwa goli moja kwani kwenye mchezo wao wa kwanza walishinda kwa 2-0
dhidi ya Malawi,huku Angola wakishinda kwa 1-0 dhidi ya Mauritius
Hivyo
mchezo huu unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa sana kwani kila
timu inahitaji kusonga mbele kwa kuzitafuta pointi 3 muhimu,mchezo
utachezwa majira ya saa mbili usiku kwa majira ya saa za Afrika
mashariki.
No comments:
Post a Comment