Taarifa
iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Leo Julai 6, 2017
inahusu kupanda na kushuka kwa viwango vya soka kwa timu za mataifa
mbalimbali,huku Tanzania ikipanda katika viwango vya soka kwa mwezi
June baada ya kufanya vizuri katika michezo kadhaa.
Tanzania imepanda kutoka nafasi ya
139 hadi nafasi ya 114, ikiwa imepanda kwa nafasi 25. Hiyo ni inakuja
kama chachu na taarifa nzuri kwa soka la Tanzania ambapo inatoa
nafasi kwa kuonesha mataifa mengine kuwa soka la Tanzania linakua kwa
kasi.
Ingawaje changamoto hazikosekani
lakini angalau sasa Tanzania imaendelea kuweka vielelezo madhubuti
katika kuinuka kisoka kadiri siku zinavyokwenda.
No comments:
Post a Comment