Msanii wa muziki, Ommy Dimpoz
ameachia wimbo wake mpya ‘Cheche’ ikiwa ni saa chache toka
atangaze kusaini katika label ya RockStar4000. Wimbo huo ameuachia
kupitia mtandao wa kuuza nyimbo za wasanii.
Muimbaji huyo kwa sasa ameungana na
Alikiba ambaye alijiunga na label hiyo miaka 6 iliyopita, ambapo wiki
iliyopita alitangazwa kuwa mmoja kati ya wamiliki wa label hiyo.
Pia label hiyo nchini Tanzania
inafanya kazi na muimbaji Lady Jay Dee pamoja na Baraka The Prince.
No comments:
Post a Comment