Timu ya taifa ya mchezo wa riadha
imeagwa rasmi leo na kukabidhiwa bendera ya taifa tayari kwaajili ya
kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia yanayo tarajiwa
kufanyika jijini London nchini Uingereza Agosti 4 mwaka huu.Timu hiyo
yenye jumla ya wachezaji nane imekabidhiwa bendera ya taifa na Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Waziri Mwakyembe amesema wizara yake iko bega kwa bega na wadau wa
michezo hapa nchini katika kuhakikisha kuwa sekta hiyo inapiga hatua.
“Kwanza kabisa nimetiwa moyo sana
na ari ya vijana waliyonayo na kama mlivyoona na kusikia kwenye
vyombo mbalimbali vya habari, vijana hawa wamepikwa vizuri na wana
ari, moyo na uzalendo mkubwa na kilicho mbele yao ni kitu kimoja tu,
kupambana kufa na kupona na kurudi na medali”
“Nilipoangalia
viwango vya vijana wa timu yetu ya taifa nilipata faraja sana. Kwani
vijana wote hawa wanaviwango vya kimataifa na ndiyo sababu wakapata
tiketi ya kushiriki michuano hii ya dunia. Hili siyo swala dogo na
napenda niwapongeze sana.
“Unaposhinda medali unapandishiwa
bendera na kupigiwa wimbo wa taifa hiyo ni heshima kubwa, vijana
wangu tukimbie hata miguu ikifika kisogoni kimbieni”.
Mara baada ya kupokea bendera ya
taifa mwanariadha, Alphonce Simbu anayeshiriki mbio ndefu za kilomita
42 amesema kuwa wao wamejiandaa kikamilifu na wanajua wanabeba
dhamana kubwa kwa watanzania wote, hivyo watahakikisha kuwa
wanapambana na kuleta medali nyumbani.
Jumla ya wanariadha wataoshiriki
mbio ndefu za kilomita 42 ni, Alphonce Simbu, Ezekiel Jafari
Ng’imba,Stephano Huche Gwandu,Sara Ramadhani Mkera, Magdalena
Crispin wote wakiwa na rekodi nzuri pia.
Wakati washiriki watatu waliyosalia
watashiriki mbio fupi, Gerald Geay,Emanuel Ginki ,Failuna Abdi
Matanga,Mashindano hayo ya dunia ya riadha yanatarajiwa kuanza Agosti
4 mwaka huu na yataendelea kwa muda wa siku 10.
No comments:
Post a Comment