Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dkt John Pombe magufuli akiwa ameambatana na mgeni wake Rais
wa Burundi,Pierre Nkurunziza aliyewasili mapema leo katka uwanja wa
mpira wa Lemela mjini Ngara,Rais Dkt Magufuli amempokea Rais
Nkurunziza akiwa kwenye ziara yake kikazi mkoani Kagera.
Aidha Rais Nkurunziza baada ya
kupokelewa na Mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli,alipata wasaa wa
kuwasalimia wananchi mbalimbali waliofika kumpokea katika uwanja huo
wa mpira mjini Ngara.
Nkurunziza ameshukuru wananchi wa
Tanzania kwa mapokezi makubwa aliyoyapata,na ameongeza kuwa sisi sote
ni wamoja na tutaendelea kuwa wamoja hivyo amepewa salamu na warundi
na atapokea salamu toka hapa Tanzania na kuzifikisha kwa raia wake,na
amemaliza kwa kumshukuru Rais Magufuli kwa kuweza kumpokea vyema.
No comments:
Post a Comment