Golikipa wa
zamani wa Young Africans {Yanga}Ally Mustafa ‘Barthez’ July 19,
2017 ametangazwa rasmi kujiunga na club ya Singida United kwa ajili
ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Barthez
amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo inayofanya
usajili wa aina yake msimu huu ukilinganisha na vilabu vingine
ambavyo havina majina makubwa nchini.
Ally
Mustafa anajiunga Singida United ambapo atakuwa katika ‘vita’ ya
namba na golikipa wa sasa wa club hiyo Said Lubawa ambapo baada ya
usajili huo Mkurugenzi wa Singida United Festo Richard Sanga
alithibitisha kubakiwa na nafasi moja ya usajili.
”Kwangu
mimi kwanza naona hakuna utofauti kati ya timu kubwa na Singida
United. Mimi naona kawaida japo kuna jina kubwa na jina dogo kwa
sababu Singida United imepanda Daraja msimu huu lakini Yanga ipo Ligi
Kuu muda mrefu na timu kubwa.”
- Barthez.
No comments:
Post a Comment