kwenye michuano ya Sportpesa Cup inayoendelea pale jijini Dar es salaam kwenye uwanja wa uhuru,
ambapo timu ya yanga Yanga imeshuka dimbani kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo ikimenyana na Timu ya AFC Leopard toka nchini kenya.
Mchezo ambao ulionekana ukiwekewa umakini mkubwa kwa timu zote,ambapo mpaka dakika tisini za mchezo matokeo yalikuwa ni sare ya bila kufungana,na ikapelekea kuingia kwenye ngwe ya matuta kwa penalti kupingwa ili kuamua mshindi wa nchezo huo.
Na hapo ndipo wana jangwani timu ya Yanga walipojikuta wakiangukia uso kwa kuwakabidhi AFC Leopard uenyeji wa michuano hiyo kwa kukosa mikwaju miwili kati ya mitano ,huku AFC leopard wakikosa mkwaju mmoja pekee,na kufanya matokeo ya mwisho kuwa 4-3.
Hivyo AFC Leopard wanasubiri mshindi kati ya timu za Kenya kati ya Gor Mahio vs Nakuru zote za kutoka nchini kenya,na kufikia kilele cha michuano hii bingwa atakayeibuka atashuka uwanjani kucheza na timu ya Everton ya nchini uingereza.
No comments:
Post a Comment