Waziri Mwigulu
Nchemba amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli
katika kuendelea kulinda rasilimali tulizonazo nchini, ameyasema hayo
alipokuwa kwenye ziara Jimboni kwake Iramba Magharibi amewaomba
Watanzania kuungana katika kumuombea Rais,na viongozi wote wenye nia
njema na moyo wa uzalendo ili juhudi za kulinda na kusimamia
rasilimali za Taifa zinazoongozwa na Rais JPM zipate mafanikio na
baraka za watanzania wote.
“Kwa mtanzania
yeyote mwenye mapenzi mema na nchi yetu lazima ataunga mkono juhudi
hizo lakini kwa ambaye ana mambo yake ya ubinafsi na ametanguliza
ubinafsi anaweza asielewe kazi inayofanywa lakini sisi ambao
tunahitaji maji; tunaohitaji barabara, tunaohitaji elimu bure,
tunaohitaji Hospitalini dawa ziwepo, tunaohitaji umeme, sote kwa
maombi na kwa jitihada na hata kwa kusema tumuunge mkono Rais wetu
kwa uzalendo na ujasiri mkubwa aliouonesha”.
“Kwa imani zetu
wote, tuendelee kumuombea Rais wa nchi yetu, Rais wetu mpendwa kwa
kazi kubwa anazozifanya ambazo zitasaidi hii mipango mingi
tunayopanga kwenye majimbo yetu, matamanio na matarajio yetu mengi
tunayokuwa nayo katika majimbo yetu”.alisisitiza Mwigulu Nchemba.
No comments:
Post a Comment