Ni burudani isiyo na kifani
imeendelea kuonekana kwenye michuano ya kombe la mabara ambapo siku
ya pili ya michuano hiyo inayoendelea huko nchini Urusi.
Katika kundi A timu ya taifa ya
Ureno walitoshana nguvu na Mexico kwa sare ya mabao 2-2, Ricardo
Quaresma alianza kuipatia Ureno goli la kuongoza katika dakika ya 35
Mexico walisawazisha goli hilo
kupita kwa “Javier Hernandez” Chicharito na kumfanya mshambuliaji
huyu kuwa ndio mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa akifikisha
mabao 48.
Beki Cedric Soares akaongeza bao la
pili kwa Ureno katika dakika ya 86 kabla ya Hector Moreno kusawazisha
goli hilo kwa upande wa Mexico katika dakika za lala salama.
Katika mchezo wa kundi B
wawakilishi wa bara la Afrika Cameroon walichapwa na mabingwa wa
Amerika ya kusini, Chile kwa mabao 2-0 mabao ya Chile yalifungwa
katika kipindi cha pili na Arturo Vidal na Eduardo Vargas.
No comments:
Post a Comment