Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim
Majaliwa amepiga marufuku usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi.
Waziri mkuu Majaliwa amesema yeyote
atakayekamatwa akijaribu kusafirisha chakula nje ya nchi hiyo,
chakula hicho kitataifishwa na kupelekwa ghala la taifa.amesema hayo
wakati akitoa nasaha kwenye Baraza la Eid lililofanyika kitaifa
kwenye msikiti wa Masjid Riadha, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro mara
baada ya kuswali sala ya Eid, waziri mkuu huyo alisema serikali
imechukua hatua hiyo kuzuia Tanzania isikumbwe na baa la njaa.
"Kuanzia leo, ni marufuku kwa mtu
yoyote kusafirisha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi bila ya
vibali. Serikali inahamasisha uwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda
nchini. Kama tutatoa vibali, ni lazima mtu alazimike kusaga nafaka
ili kutoa ajira nchini,” akaongeza kwa kusema " Mimi nasema
kuanzia leo, yeyote atakayekamatwa akitorosha chakula kwenda nje ya
nchi, chakula hicho kitataifishwa na kupelekwa ghala la Taifa na gari
lake tutalitaifisha na litaishia Jeshi la Polisi. Tunafanya hayo kwa
lengo la kuwalinda Watanzania tusikumbwe na baa la njaa”.
Ametanabaisha kuwa mipaka ya
Tarakea, Holili, Mwanga, Horohoro, Siha, Namanga na Sirari imekuwa
inapitisha kiasi kikubwa cha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi
jambo ambalo ni hatari sana. Lakini pia waziri mkuu huyo amewataka
wafanyabiashara wa ndani ya nchi ya Tanzania, wachukue mahindi kutoka
maeneo yenye mavuno mengi na kuyapeleka kwenye sehemu zenye mavuno
kidogo.
No comments:
Post a Comment