Waziri wa mambo ya ndani wa
Tanzania Mwigulu Nchemba amesema kama kuna taasisi yoyote imesajiliwa
nchini na inafanya kampeni za haki za ushoga basi atafuta usajili huo
na watu wake kukamata na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
"Wanaotaka haki za ushoga
watafute tu nchi yao nyingine ambayo inaruhusu mambo hayo wakakae
huko, kama ni taasisi imesajiliwa kwenye nchi yetu tukaigundua
inafanya kampeni ya haki hizo na bahati nzuri zinasajiliwa Wizara ya
Mambo ya Ndani nitazifutia usajili wao”.
"kama ni raia wa Tanzania
anaendesha kampeni hizo tutamkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya
sheria, na kama si raia amekuja kwenye nchi yetu kuja kuendesha haki
hizo tutampa amri ya kuondoka ndani ya nchi yetu hatapata fursa hata
ya kuchomoa chaji ya simu kwenye soketi ya umeme”.
Pia
Waziri Nchemba ameunga mkono kauli,na maelekezo ya Rais Magufuli
dhidi ya wanafunzi ambao watapata ujauzito wakiwa shuleni na kusema
watu wanaopinga jambo hilo wasitumie nguvu kubwa kupinga bali wajenge
shule zao watoe hiyo haki ya kusomesha wanafunzi wajawazito au wale
ambao tayari wamejifungua na siyo kulazimisha serikali kufanya hayo.
No comments:
Post a Comment