Michuano
ya Cosafa castle cup,ambayo inaendelea huko Afrika kusini huku Taifa
Stars wakiwa ni waalikwa kwenye michuano hiyo ambapo leo hii
wameshuka dimbani kucheza na timu ya Malawi,huku Taifa stars
wakionesha makali katika kipindi cha kwanza cha mchezo kwakuweza
kuwachapa goli mbili zilizofungwa na Shiza Kichuya.
Nacho
kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku malawi wakiweka jitihada
katika kutafuta magoli,lakini vijana wa taifa stars walionekana
kusimama imara kwa kuweza kulinda magoli waliyoyapata.
Hivyo
kufanya matokeokubaki kama yakipindi cha kwanza kwa timu ya taifa ya
Tanzania Taifa Stars kuibuka kidedea kwa kunyakua point 3 muhimu na
magoli 2-0 mkononi,kwenye mchezo wao wa kwanza ya michuano hiyo
kwenye kundi A.
No comments:
Post a Comment