Tuzo za Bet ambazo zimetolewa
usiku wa june 24, 2017 mjini Los Angeles, katika ukumbi wa Microsoft
Theater Centre, Rayvanny ambaye alikuwa akiwania tuzo hizo kupitia
kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act
amefanikiwa kuibuka kidedea.
Wasanii wengine ambao alikuwa
akishindana nao katika kipengele hicho ni Dave (Uingereza), Amanda
Black (Afrika Kusini), Changmo (Korea Kusini), Daniel Caesar, Remi na
Skip Marley (Jamica).
Baada ya kushinda tuzo hiyo, Ray
kupitia mtandao wake wa Instagram ameshukuru kwa kuandika, “God is
good all the time.Asante Mungu wangu Ulieniumba,Unaejua mwanzo na
mwisho wangu.Uliyaona machozi yangu nilipokua mpweke sina furaha na
mwenye majonzi mengi.WEWE NDIYE MUWEZA…”
“Asanteni wadau Wote mlio VOTE
kwa Ajili yangu Ushindi umerudi Nyumbani.SITOACHA KUSHUKURU UONGOZI
MZIMA #WCB @babutale @sallam_sk @Diamondplatnumz @mkubwafellatmk
@kameboy_j @ricardomomo thanks Alot @bet_intl @betawards @bet_africa
#WCBFORLIFE MAMA I LOVE YOU,” ameongeza
No comments:
Post a Comment