Michuano ya soka ya mabara
imeendelea kushuhudiwa pale nchini Urusi ambapo michezo miwili
imepigwa ili kuzipata timu za kuingia nusu fainali.Hatimae wenyeji wa
michuano hiyo Urusi wamecheza dhidi ya timu ya Mexico ambapo
ilishuhudiwa waandaaji hao wa michuano hiyo kwa mwaka huu wakitupwa
nje ya michuano hiyo.
Mexico waliibuka kidedea kwa
ushindi wa mabao 2-1, ingawaje Urusi ndio walitangulia kucheka na
nyavu za Mexico katika dakika ya 25 kupitia kwa Aleksandr Samedov
kabla ya Nestor Araujo kusawazisha dakika ya 30.
Kwenye kipindi cha pili Mexico
walionekana kuja na kasi nzuri iliyowawezesha kupata bao la ushindi
dakika ya 52 kupitia kwa Hirving Lorzano hivyo mchezo ukamalizika wa
Mexico kusonga mbele kwenye hatua inayofuata huku wenyeji wakijawa na
simanzi.
Mabingwa wa Ulaya Timu ya taifa ya Ureno waliokuwa wakicheza na vibonde wa Newzealand ambapo Ureno walishusha kipigo cha mbwa mwizi kwa kuinyuka Newzealand bao 4-0.wachezaji walioipatia Ureno ushindi ni “Ronaldo, Bernardo Silva ,Andre Silva, Louis Nani”, Matokeo haya yanazibebe Ureno na Mexico kuelekea nusu fainali kwa kusubiria matokeo ya timu zitakazofuzu hatua hiyo toka kwenye kundi B.
No comments:
Post a Comment