Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe
ameridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa eneo la kuchezea mpira
(picth) la Uwanja wa Taifa wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es
Salaam.
"Nimefurahishwa na mabadiliko
niliyoyaona katika hatua hii ya awali naamini ukarabati
utakapokamilika milango itakuwa wazi kwa mechi za kimataifa ikiwemo
mashindano ya AFCON yanayoratajiwa kufanyika nchini kwetu mwaka 2019" alisema kwa kuongeza kuwa Serikali ipo katika mkakati wa kuhakikisha
viwanja vingine vikiwemo vya mikoani vinafanyiwa ukarabati ili
kuboresha sekta ya michezo nchini. Alisema Waziri Mwakyembe.
Uwanja
wa Taifa ulianza matengenezo ya eneo la kucheze (pitch) rasmi
katikati wa mwezi wa sita lengo ni kuhakikisha nyasi zilizochakaa
zinaondolewa na kuwekwa nyasi mpya zitazodumu zaidi ya miaka 10.
No comments:
Post a Comment