Msanii na mwimbaji wa Bongofleva
Vanessa Mdee”V Money” akiwa kwenye kipindi cha XXL ya Clouds FM
leo juni 16 2017 amesema kuonekana kwake kwenye video akiwa
anawabusu mwanaume ni sehemu ya kazi tu na si vinginevyo.
Vanessa ameyasema hayo wakati
anaelezea namna alivyoonekana kwenye Red Carpet ya tuzo za Billboard
na jinsi alivyopata deal la kuigiza Tamthiliya ya Shuga na kuelezea
namna alivyoonekana akikiss na mwanaume mwingine kwenye Tamthiliya
hiyo.
Jamani ile ni kazi,Halafu mimi ni
muigizaji na Kwenye Shuga nimeigiza na hiyo show ina mafunzo kama mtu
akiangalia kwa makini atajifunza kitu kikubwa sana.Nawasihi wadogo
zangu na Watanzania wakaiangalie watapata kitu.
“Hata Jux anajua kuwa ile ni
kazi,kwani hata nae ,huwa inatokea akiwa na mademu wake huko kwenye
ma-video wanashikana shikana,kwahiyo sio kama nalipiza la hasha,
sema kila kitu kwenye maisha kimegusa sanaa na sanaa imegusa
maisha.”aliongeza Vanessa.
No comments:
Post a Comment