Michuano ya mabara"Confedaration
Cup” inayoanza siku ya leo june17 nchini Russia,ambapo wenyeji
Russia watachuana na New Zealand kwenye mchezo wa ufunguzi wa
mashindano hayo.
Mchezo huu kati ya Russia na
NewZealand unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa St Petersburg uwanja
wa nyumbani wa klabu ya St Petersburg.
Timu ya taifa ya Ureno
wataliwakilisha bara la Ulaya kama mabingwa wa bara hilo huku
waandishi wa habari wakiwa wamepiga kambi katika timu hiyo kufuatilia
mkasa mkubwa wa kodi unaomuandama Cristiano Ronaldo.
"Ronaldo ameonekana kuichukulia
umuhimu michuano hii na hawazi yanayotokea nje ya uwanja kwani akili
yake yote iko katika michuano hii tu"
Inasemekana tangu ishu ya
Cristiano Ronaldo kusemekana anakwepa kodi kutawala vyombo vya
habari ,Jamaa ameonekana kukosa raha na huenda anafikiria kuondoka
nchini Hispania kwenye klabu yake ya Real Madrid,june18 ureno
watashuka dimbani dhidi ya Mexico.
No comments:
Post a Comment