Mbunge
wa Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka alisimama Bungeni mjini Dodoma
mwishoni mwa wiki kuchangia kwenye Bajeti Kuu ya Serikali
inayoendelea kujadiliwa kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Aidha
ameomba serikali iwaangalie watu wa kagera kwa jicho la tatu hasa
kwenye bidhaa zote zinahusika kwenye vifaa vya ujenzi,ili watu wa
kagera waweze kujenga na kufanya marekebisho ya nyumba zao
zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi.
Ameshukuru
pia kwa kuondolewa kwa kodi kadhaa kwenye mazao,pia mabenki
yamewezeshwa lakini pia tuangalie zaidi kwa upande wa bima ili ziwe
msaaada mkubwa zaidi kwa watu wetu.
Ameomba
pia serikali iendelee kutoa ruzuku mbalimbali kwenye maeneo tofauti
hasa kwenye eneo la kilimo,amesema bajeti ni nzuri na imelenga
kuwasaidia watu wa chini kwa kiwango cha juu,hivyo huenda ikaleta
tija kwa maendeleo ya taifa.
No comments:
Post a Comment