Tanzania imeendelea kuonekana ni
moja ya nchi zinazoendelea kukua kiuchumi kwa kasi ,na kwa kupitia
ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia (WB) na imewekwa list ya nchi
ambazo zinakuwa haraka kiuchumi mwaka 2017 hasa kwa kuonekana
kuimarisha biashara na miundombinu.
Katika list hii Ethiopia inakamata
nafasi ya kwanza ambapo uchumi wake umekua kwa 8.3% huku Tanzania
ikitajwa miongoni mwa nchi 10 ikikamata nafasi ya 5 uchumi wake
ukikua kwa 7.2% huku uchumi wa Djibouti ukikua kwa 7% licha ya
kukabiliwa na ukame mkubwa.
"Baaada ya kuwepo kwa taarifa iliyoionesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unaendelea kukua kwa kasi duniani,wadau mbali mbali wameeleza huenda usimamizi mzuri wa rasilimali kwenye awamu ya tano ya uongozi wa nchi hiyo huenda ndio ukawa ni chachu ya kuinuka kwa uchumi".
"huku ikitajwa kuwa harakati za kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi vimezidi kuimarisha utendaji kazi na msukumo wa kizalendo miongoni mwa watumishi na raia wa taifa hilo,lililopo Afrika ya mashariki".
No comments:
Post a Comment