Mchezo wa ufunguzi ya hatua ya
makundi michuano ya Ndondo Cup 2017 Makuburi SC vs Stim Tosha
imemalizika kwa sare na kupelekea timu hizo kugawana pointi,mchezo
ulikuwa ni wa hali ya juu huku kila timu ikiliandama goli la mwenzake
ili kuzitafuta pointi tatu.
Shangwe kubwa toka kwa Mashabiki
waliojitokeza kwenye uwanja wa Kinesi kwa ajili ya kushuhudia pambano
hilo ambapo kulikua na burudani kibao kutoka kwa wasanii wa muziki wa
Kisingeli (Sholo Mwamba, Man Fongo pamoja na Moto Kombati “mwendo
wa mateka”
Mashabiki waliweza kuonesha
ustaarabu na nidhamu nzuri wakati wa mchezo na hata baada ya mchezo
na imepelekea kuonesha utofauti mkubwa ,kwani wengi wamekua
wakiamini Ndondo ni sehemu ya fujo na vurugu.lakini ndondo imeendelea
kudhihirika kuwa ni sehemu ya burudani kwa wapenda michezo na
burudani.
No comments:
Post a Comment