Nchini Ureno kumezuka moto mkubwa
wa msituni katika maeneo ya katikati mwa nchi hiyo, na kusababisha
vifo vya zaidi ya watu 25 na kuwajeruhi wengine 20, wakiwemo maafisa
kadhaa wa zima moto.
Awali watu waliofariki walikuwa 19,
lakini sasa idadi hiyo imepanda na kufikia 25. Wengi wao walifariki
pale walipokuwa wakiukimbia mji wa Pedrogao Grande,na kuendelea
kuvuta hewa yenye moshi mkali umbali wa kilomita 50 Kusini mashariki
mwa Coimbra, wakitumia magari yao.
Waziri wa maswala ya ndani wa nchi
hiyo João Gomes, amewaambia waandishi habari kuwa, waathiriwa 16
wameteketea ndani ya magari yao hadi kufa, pale walipokabiliwa na
moto huo mkubwa katika Wilaya ya Pedrógão Grande barabara
inayounganisha miji ya Figueiro dos Vinhos na Castanheira de Pera.
Haijabainika kilichosababisha moto
huo wa msituni, ambao umeteketeza nyumba nyingi katika maeneo hayo na
tayari baadhi ya nchi zilizoguswa na kutokea kwa janga hilo zimeanza
kutoa msaada kwa kushirikiana ili kukabiliana na moto huo huku nchi
kama Hispania ilituma ndege za kusaidia kuzima moto huo.
No comments:
Post a Comment