Timu ya taifa ya Ujerumani leo
walikuwa uwanjani katika mchezo wao wa kwanza wa michuano ya
Confedaration Cup dhidi ya timu ya taifa ya Australia.
Mchezo huo ulionekana kuwa na
upekee ambapo Ujerumani walitangulia kupata bao la kwanza dakika ya
5 kupitia kwa Larsi Standi kabla ya Tom Rogic kuisawazishia Australia
dakika ya 41 na dakika ya 45 Julian Draxler aliipatia Ujerumani bao
la pili.
Kipindi cha kwanza kiliisha kwa
Ujerumani kuongoza bao 2 kwa 1 na katika kipindi cha pili dakika ya
48 Leon Goreztka aliiandika Ujerumani bao la 3 kabla ya Tomi Juric
kuipatia Australia bao la pili.
Matokeo hayo yanaifanya Ujerumani
kuwa na pointi sawa na Chile ambao jana waliifunga Cameroon huku
Australia na Cameroon wenyewe wakikosa pointi muhimu mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment