Taifa Stars imealikwa kwenye
michuano iliyoandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini
mwa Afrika,ambapo Tanzania sio mwanachama wa Cosafa, lakini imepata
mwaliko katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka
huu.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Taifa
Stars, Salum Mayanga, kikosi kinachoondoka leo ni makipa Aishi Salum
Manula (Azam FC), Benno David Kakolanya (Young Africans SC) na Said
Mohammed Said (Mtibwa Sugar FC).
Safu ya ulinzi wapo: Shomari Salum
Kapombe (Azam FC) na Hassan Hamis Ramadhan ‘Kessy’ (Young
Africans SC) wakati upande wa kushoto wapo Gadiel Michael (Azam FC)
na Amim Abdulkarim (Toto Africans FC), Erasto Nyoni (Azam FC), Salim
Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona
(Tanzania Prisons) wakati viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam
FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC.
Upande wa viungo wapo: Mzamiru
Yassin Selembe (Simba), Simon Happygod Msuva (Young Africans SC),
Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza Ramadhani Kichuya (Simba SC).
Nayo safu ya ushambuliaji wapo:
Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Abeid Yusufu
(Kagera Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani
Idd Chilunda (Azam FC).
No comments:
Post a Comment