Dkt Magufuli akiwa kwenye ziara
yake ya siku tatu mkoani Pwani amewaambia wanachi wa mkoa huo kuwa
kwa mtoto wa shule ni marufuku kupata mimba kisha kuendelea na shule.
"Mtu amezaa iwe kwa makusudi iwe
kwa raha zake akienda shuleni si atawafundisha wenzie? Yaani
tusomeshe wazazi.Katika utawala wangu hakuna aliyezaa atakayerudi
shuleni.” Hawa watu watazaaa mno, sababu huo mchezo ni mzuri,
katika kipindi changu kama Rais ukipata mimba kwaheri.Mwisho utakuta
darasa la kwanza wote wana watoto wanawahi kunyonyesha,kwasababu
mchezo huu ni mzuri.Hizo NGO’s zitalipeleka taifa pabaya na hao
sijui na wenyewe wakafungue shule za wazazi, siyo zilazimishe
serikali kusomesha wazazi"alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli alisema
waliozaa shuleni wanaweza kwenda kupata elimu nyingine kama vyuo vya
ufundi stadi (Veta) anaweza akajifunza kushona cherehani anaweza
akaenda kukopa akaanza kilimo cha kisasa anaweza akafanya shughuli
nyingine.
No comments:
Post a Comment