Michuano ya Sports Extra Ndondo Cup
imeendelea kwenye viwanja tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam
ambapo Kwenye uwanja wa Kinesi, Mdandu Investment walichuana na Kibo
Kombaini. na wamepata ushindi wa magoli 2-1.
Magoli yote ya Mdandu yamefungwa na
mkongwe Kudra Omary dakika ya 8 na 18 kipindi cha kwanza wakati bao
la Kibo Kombaini likifungwa na James Msuva dakika ya 45 kipindi cha
kwanza.
Huko Kwenye uwanja wa Tandika
Mabatini,umechezwa mchezo mwingine ambao umewakutanisha baina ya
Kibada One dhidi ya FC Madiba,na mwishowe kibada wameibuka na ushindi
wa magoli 4-3.
Lakini
pia kwenye uwanja wa Airwing Burudani FC wameibuka na ushindi wa
magoli 2-1 dhidi ya Inter Twiga.
No comments:
Post a Comment