Mbunge wa Jimbo la
Mtama, Mhe. Nape Mnauye akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwa kufanikisha kuandaa Bajeti ya
kihistoria ya shilingi trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha
2017/2018,iliyopitishwa mjini Dodoma
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb), akimpongeza
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwa
kufanikisha kuandaa Bajeti Kuu ya Serikali ya kihistoria ya shilingi
trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Mbunge wa Jimbo la
Misungwi, Mhe. Charles Kitwanga akimkumbatia kwa furaha,Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kwa kufanikisha
kuandaa na hatimaye kupitishwa kwa Bajeti ya kihistoria ya shilingi
trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiteta kidogo na maafisa waandamizi wa Wizara yake nje ya ukumbi wa Bunge mjini
Dodoma, baada ya Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali
ya shilingi trilioni 31.7.
No comments:
Post a Comment