Mh Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ameendelea na ziara yake mkoani pwani kwenye siku ya pili ya ziara hiyo.
Ambapo ametembelea kiwanda cha
Global Packaging na kuzindua kiwanda hicho ikiwa ni sanjari na
kuangalia namna kinavyofanya kazi,na mandhari nzima katika hatua za
uzalishaji wa bidhaa za kiwanda hicho.
Kiwanda hicho kilichopo eneo la
Kibaha kinajishughulisha na uzalishaji wa vifungashio,ambavyo ni
mifuko maalumu ianyotumiwa na watu mbalimbali katika kuhifadhi mazao
mbalimbali,zaidi kama vile maharge ,mahindi,dengu na kadhalika.
Rais Dkt. Magufuli akiwa na vingozi
wenzake ikiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage,
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Mkuu wa Mkoa wa
Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo akipata maelekezo mara baada ya
kufungua kiwanda cha vifungashi cha Global Packaging (T) LTD mjini
Kibaha asubuhi hii ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu
ya mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment