Raisi wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli awahutubia
wananchi wa mkoa wa pwani maeneo ya kibaha maili moja,kwenye siku ya
kwanza ya Ziara yake kwenye mkoa huo,leo hii juni 20 2017.
Hakika
wanachi walionekana kuvutiwa na ziara hiyo ya Raisi Magufuli kwani
waliweza kujitokeza kwa wingi,na kuyafanya mapokezi hayo kuwa makubwa
lakini pia waliweza kuonesha imani kwa Raisi wao.
Ameendelea
kulia na wale wote wanaotaka kuharibu mali za taifa hili,amewaomba
wananchi kuendelea kumuunga mkono kwani kama kero za wananchi hazina
vyama,hivyo ili taifa liende mbali ni lazima rasilimali ziangaliwe na
kusimamiwa kwa umakini mkubwa ili taifa liweze kujiendesha kiuchumi.
Japokuwa
changamoto ni nyingi,lakini bado tunaendelea kuzimaliza taratibu na
tuna uhakika zitamalizika na mambo kuwa sawa ili watanzania wa hali
ya chini waendelee kuona mema na neema za nchi hii.na hili najua
tutakubaliana kuwa tumeziba mianya ya ubadhilifu,tumeendelea
kusimamia wakwepa kodi kulipa ili tuijenge nchi kwa kiwango ambacho
katika utawala wa awamu yangu naamini watu watajua kwanini
tutaendelea kusisitiza watu kuwa wazalendo.
No comments:
Post a Comment