Ndondo Cup 2017 imeendelea leo kwenye
uwanja wa Tandika Mabatini kati ya Kauzu FC dhidi ya Sheraton FC,
ambapo Kauzu waliibuka kidedea na ushindi wa mabao 2-1.
Kauzu walipata bao la kwanza dakika
ya 5 mfungaji akiwa ni “Hamad Kibopile” dakika 23 Kauzu wakafunga
bao lao la pili likifungwa na “Awadh Said” na kuwafanya Kauzu
kwenda mapumziko na akiba ya magoli hayo 2 kwa 0.
Kwenye kipindi cha pili Sheraton
walijipanga na kuongeza kasi katika mchezo kwa kulisakama goli la
wapinzani na kufanikiwa kufunga goli dakika ya 56,hivyo kuwafanya
wakaambulia goli moja la kufutia machozi na kuwaachia Kauzu pointi 3
muhimu.
Na game nyingine ilikuwa ni kati ya
“ Faru Jeuri” dhidi ya “Miami” kwenye uwanja wa Benjamini
Mkapa mchezo ambao umemalizika kwa timu hizo kutoa sare bila
kufungana.
No comments:
Post a Comment