Tanzania ni nchi inayohifadhi
wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine katika
ukanda wa Afrika Mashariki,Ripoti ya shirika la wakimbi la Umoja wa
Mataifa UNHCR inasema hadi hivi sasa, kuna wakimbizi Laki 2 na 41
elfu waliopo kwenye kambi za wakimbizi nchini Tanzania wanatokea
Burundi.
Ripoti iliyoainisha kati ya kipindi
cha miezi mitano,ya mwaka huu 2017, wakimbizi 44,487 wamekimbilia
Tanzania wakitokea Burundi.UNHCR imegundua kuwa Tanzania inakumbana
na mzigo mkubwa kwa kuwahudumia wakimbizi hawa ilhali hawapati fedha
za kutosha kuwahudumia wakimbizi na wengine wanaotafuta hifadhi.
Kambi moja kwa mfano ya Nyarugusu,
ambayo inatajwa kuwa ni moja ya kambi kubwa za wakimbizi duniani,
inahifadhi wakimbizi 139,0000 idadi ambayo inapaswa kupunguzwa na
kuwagawa wakimbizi katika kambi nyingine.
Hata hivyo serikali ya Tanzania
imesifiwa kwa kuendelea kubeba mzigo huu mkubwa wa wakimbizi lakini
zaidi kwa kukubali kutekeleza mkakati mpya wa kimataifa ujulikanao
kama COMPREHENSIVE REFUGEE RESPONSE.
Mkakati huu unalenga kutafuta namna
endelevu ya kuwasaidia wakimbizi kupata ulinzi na mahitaji mengine ya
msingi ya kibinadamu, lakini zaidi sana kutafuta namna ya
kuwashirikisha wakimbizi hawa katika shughuli mbali mbali za
maendeleo katika nchi wanazokimbilia.
No comments:
Post a Comment