Mabingwa wa soka Tanzania bara kwa mara tatu
mfululizo klabu ya Yanga wamepatwa na msiba mzito baada ya moja ya
aliyekuwa mshabiki wao nambari moja kufariki.
Shabiki huyo aliyekuwa akitambulika kama
Ally Yanga amefariki hii leo mchana jijini Dodoma ambako taarifa
zinasema alikuwa kwenye shughuli za kukimbiza mwenge,Ally Yanga
alipata umaarufu sana kwa ushangiliaji wake wa kipekee kwa kujipaka
“masinzi” ya mkaa usoni na kujaza nguo katika tumbo lake kama ana
kitambi.
Kutokana na msiba huo aliyekuwa msemaji wa
klabu ya Simba bwana Haji Manara ametuma salamu za pole kwa watani
wake hao na akisema amehuzunishwa na msiba huo. “nimepigiwa
simu kwamba Ally Yanga amefariki huko Mpwapwa mkoani Dodoma,msiba huu
ni wetu wote na tunawapa pole watani zetu.” aliandika
Manara kwenye instagram akaunti yake.
No comments:
Post a Comment