Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona
Lionel Messi na baba yake,wamenusurika kwenda jela baada ya
kupatikana na hatia katika kesi iliyokuwa ikiwakabili ya ukwepaji
kulipa kodi,na kutakiwa kulipa faini ikiwa ni mbadala wa vifungo
vyao.
Mwezi Julai mwaka jana Lioneil
Messi na baba yake walikutwa na hatia katika kesi hiyo iliyokuwa
ikiwakabili na baada ya hukumu waliamriwa kulipa faini au kutumikia
kifungo.Messi na baba yake walihukumiwa kifungo cha miezi 21.
Messi na baba yake waliajiri kundi
la mawakili ambao walijaribu kuwatete katika kesi hiyo bila mafanikio
na baadae mamlaka za kisheria zikawahukumu.Sasa taarifa zinasema
Lioneil Messi amekubali kulipa faini ya euro 252,000 na baba yake
akilipa euro 180,000 na hiyo itawafanya kuepuka kifungo kilichokuwa
kinawakabili.
Masta kadhaa wa soka wamekuwa
wakikumbwa na tuhuma za ukwepaji kodi nchini Hispania ambapo
Cristiano Ronaldo na kocha Jose Mourinho nao wapo katika uchunguzi.
No comments:
Post a Comment