Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM
katika kuhakikisha linadumisha amani na hali ya usalama na utulivu
kwenye msimu huu wa Sikukuu limesema litatumia vikosi vyake vyote
kusimamia amani na usalama maeneo mbalimbali zikiwemo kumbi na sehemu
zenye mkusanyiko wa watu wengi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari,
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM Lucas Mkondya amesema Jeshi
hilo limejipanga kuhakikisha Watanzania wanasherehekea vizuri Sikukuu.
"Napenda
kuwaambia kwamba Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM tumejipanga
vyema sana. Kwa hiyo Wananchi wajiandae tu kwa sherehe,Nyumba zote za
Ibada tutaweka Askari. Kutakuwa na Askari wa kawaida wenye Uniform
lakini pia kutakuwepo na Askari kanzu kufuatilia nani anataka kufanya
vurugu katika nyumba za Ibada lakini pia katika sehemu ambazo
Wananchi wataenda kufanya Sherehe".
"Tunawaomba
wananchi wawachunge watoto wao,madereva wasinywe pombe na wasingatie
sheria za usalama barabarani pindi waendeshapo vyombo vyao vya
moto,na wanaopendelea kwenda beach wawe makini na watoto,lakini pia
wamiliki wa kumbi za starehe ni marufuku kuweka disko toto na
watakaokiuka maelekezo watachukuliwa hatua kali mara moja".
"Tutatumia
katika kuhakikisha ulinzi unaimarika tutatumia Vikosi vyetu vyote.
Tutatumia Vikosi vya FFU vitakuwepo mitaani kwa ajili ya kuimarisha
Doria. Tutatumia Helkopta, tutatumia Farasi, tutatumia Mbwa na Askari
wengi sana watakuwepo. Kwa hiyo napenda kuwahakikishia Wananchi
kwamba wasiwe na wasiwasi Jeshi lao la Polisi limejipanga katika
kuwalinda na kuhakikisha kwamba Sikukuu Eid Mosi, Eid Pili zinapita
salama bila kubughudhiwa." aliongea kaimu kamanda wa
kanda maalumu Dsm -Lucas Mkondya.
No comments:
Post a Comment