Mabingwa watetezi wa kombe la
Ndondo Cup Temeke Market wamechezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa
Makuburi SC kwenye mchezo wa Kundi G uliopigwa kwenye uwanja wa
Kinesi pale maeneo ya Sinza Dar es Salaam.
Mwinyi Ally alianza kuifungia bao
Makuburi dakika ya 56 kipindi cha pili baada ya timu hizo kumaliza
kipndi cha kwanza bila kufungana, Paul Ndauka akaisawazishia Temeke
Market dakika ya 70 lakini wakati zimesalia dakika nane tu mechi
imalizike Victor Hangaya akaifungia Makuburi bao la ushindi.
Katika uwanja wa Mwl. Nyerere,
Magomeni, Dar Police Collage wamepoteza mechi yao ya pili mfululizo
kwenye Kundi G baada ya kufungwa 1-0 na Stim Tosha timu kutoka maeneo
ya Mabibo. Dar Police Collage wamejiweka kwenye wakati mgumu wa
kusonga mbele kwenye michuano hiyo wakiwa hawana hata pointi hadi
sasa baada ya kucheza mechi mbili.
No comments:
Post a Comment