Usiku wa June 3 2017 jijini Cardiff
nchini Wales ilikuwa ni siku ya kihistoria katika uwanja wa Millenium
mahali ambapo anatokea staa wa Real Madrid Gareth Bale, usiku huo
Real Madrid walicheza game yao ya fainali ya UEFA Champions League
dhidi ya Juventus.
Real Madrid ambao ndio walikuwa
Mabingwa watetezi wa taji hilo wamefanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara
ya pili mfululizo baada ya kuifunga Juventus magoli 4-1,Cristiano
Ronaldo ambaye ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufunga
jumla ya magoli 12 alifunga magoli dakika ya 20 na 64.
Casmiro ndio alikuwa staa wa Real
Madrid aliyefunga goli la pili dakika ya 61 na Asensio akafunga goli
la nne dakika ya 90, Juventus walifanikiwa kupata goli la kwanza
dakika ya 27 kupitia kwa Mandzukic na kuufanya mchezo huo kwenda
mapumziko magoli yakiwa 1-1.
Ushindi huo sasa unaiwekea Real
Madrid kuendelea kuwa club iliyotwaa mataji mengi ya Champions League
kwa kutwaa taji la 12, AC Milan wao wanaendelea kuwa nafasi ya pili
kwa kutwaa taji hilo mara 5, Ronaldo anaendelea kuweka rekodi ya
kumfunga Buffon goli 7 wakikutana kwa mara ya 5 wakati mpinzani wake
Messi ameshindwa kumfunga Buffon hata mara moja.
Kufunga magoli mawili kwa Ronaldo
kumemfanya kufikisha jumla ya magoli 600 katika maisha yake ya soka
akifunga kwa ngazi ya club na timu ya taifa, Ronaldo pia anaendela
kuwa mchezaji pekee aliyewahi kufunga magoli kuanzia 10 katika
michuano ya Champions League katika misimu sita mfululizo, Real
watacheza na Man United August 8 UEFA Super Cup.
No comments:
Post a Comment