• DON'T MISS

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****
    RABA CLASSIC

    Thursday, 1 June 2017

    Kiungo wa Azam Himid Mao aeleza mkataba wake na Azam,na majaribio yake Denmark.

    Himid Mao, kiungo wa ulinzi wa Azam FC na timu ya taifa ameeleza majaribio aliyokwenda kufanya Denmark kwenye klabu ya Randers yalienda vizuri na anachosubiri sasa ni makubaliano ya timu yake ya Azam na klabu hiyo ya Denmark.

    Nilifanikiwa majaribio na timu yao na nilifanikiwa kucheza baadhi ya mechi pia, kwakuwa wameshaniona kilichobaki ni wao kumalizana na uongozi wa Azam ili niweze kujiunga nao.”

    Mawasiliano na majadiliano bado ya yanaendelea wakala wangu ananipa ripoti kwa kila hatua inayopigwa watanzania wawe na subira chochote kinaweza kutokea na nitakuja kuweka wazi mambo yatakavyokuwa”.

    Aliongeza kuwa alikuwa akifuatiliwa kwa muda mrefu haikuwa kama bahati, “sports director wao alikuwa ananifuatilia kuanzia kwenye mechi za Azam na timu ya taifa kwa hiyo ni watu ambao wananifahamu vizuri.” amemaliza kwa kutanabaisha kuwa mkataba na Azam unamalizika mwezi november hivyo ofa zitakazokuja atachagua moja itakayomfaa.

    No comments:

    Post a Comment