Msanii Lava lava amezungumza kwenye
kipindi cha Papaso cha TBC Fm, kwa kusema WCB ni familia ambayo
inafanya kazi kwa ushirikiano na kuelekezana hivyo suala la
kufunikana halipo.
“Wasanii wa WCB wote ni wakali
kwenye kazi, tena ukikaa unasema hii sehemu nitapitaje hapa lakini
mwisho wa siku kitu ambacho kinanipa moyo ni kwamba hadi umeona
uongozi umekaa na kuamua kunitoa mimi kunipeleka mbele za watu ujue
kuna kitu kwangu. Msanii yeyote wa WCB nipo tayari kufanya nae kazi…
kufunikwa ni sehemu ya kujipima, ila mwisho wa siku kila mtu ana
mashabiki wake,” aliongea Lava Lava
Lava Lava ambaye anakamilisha idadi
ya msanii wa tano kujiunga na Lebo ya WCB ambapo wengine
waliotangulia ni Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen na Rich Mavoko.na
msanii huyu amekuja vizuri kwenye muziki kwani Wimbo wake wa kwanza
kutoa unaitwa “Tuachane” unafanya vizuri sana kwenye media
kwa sasa.
No comments:
Post a Comment