Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania DtkJohn Pombe Magufuli amesema kuanzishwa kwa mfumo mpya wa
serikali wa ukusanyaji kodi kwa njia ya Kielekroniki, (Data Center)
itakuwa dawa kwa wote wanaokwepa kulipa kodi.
Ameyaongea haya alipokuwa akizindua
uanzishwaji wa mfumo huo,ambapo pia anaamini mfumo huu utasaidia
kuondoa malalamiko ya wale wanaodai kubambikiziwa kodi isiyo na
uwiano,lakini hata wale wanaokwepa kulipa kodi ufumbuzi ni huu wa
kuwepo kwa kituo hicho.pia amesisitiza wafanyabiashara na makampuni
kuingia katika mfumo huu ili kukwepa udanganyifu kwa ustawi wa nchi.
Lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho
ni dhamira ya serikali ya Tanzania katika kukuza na kuimarisha sekta
ya Teknolojia na Habari na mawasiliano ambayo inakuwa kwa kasi
ulimwenguni kote na ni kichocheo kikubwa cha uchumi.lakini kudumisha
muungano ni sehemu ya mpango huo kwani tozo zote zitakuwa wazi katika
kutanabaisha walipa kodi kwa pande zote mbili Jamhuri ya muungano wa
Tanzania.
No comments:
Post a Comment