Kenya imezindua reli mpya kati ya
mji wa Mombasa hadi Nairobi,Reli hiyo imetengezwa kwa ufadhili wa
toka serikali ya China.
Mradi huo mkubwa kimiundombinu
umechukua takriban miaka mitatu na nusu kwa kutumia teknolojia ya
ujenzi wa reli ya China,Reli hiyo inatarajiwa kuunganisha Sudan
Kusini, DR Congo ,Burundi na Mombasa.
Safari ya kutoka Mombasa kuelekea
Nairobi na treni ya kisasa itachukua saa nne na nusu ikilinganishwa
na saa tisa kwa kutumia basi na saa 12 kwa kutumia treni ya
zamani.Nauli ya watu watakaokalia viti vya kawaida ni shilingi 900
huku wale watakaosafiri kwa kutumia business class wakilipa shilingi
3,000.
Serikali ya kenya imeendelea
kuimarisha miundombinu katika kuhakikisha wanawavutia wawekezaji
wengi kuja kuwekeza nchini humo,ambapo wameendelea kuamini Madaraka
Express itawasaidia katika kufikia malengo muhimu.
No comments:
Post a Comment