Ameanza kwa kuwashukuru waandishi wa habari kwa kutenda kazi zao
vizuri,kwa habarisha watanzania,ameomba kuendeleza ushirikiano
waliouonesha hapo awali kwa Igp aliyepita,amemshukuru Rais kwa
kumteua katika nafasi hiyo.
Ameeleza hali ya usalama nchini bado iko sawa,japo kuna maeneo
machache kama rufiji ambapo amesema hatotaka kuzungumza bali majibu
yatapatikana.
" Salamu kwa hilo kundi la watu wachache,ambao wanatengeneza
na kufanya mabaya basi ubaya wao utarudishwa kwa ubaya wa kisheria
zaidi".
"Ameeleza kuwa kundi la bodaboda ambao wamee,ambao wameanza kufunja
sheria kwa makusudo waache mara moja,ameonya pia watu wanaojiita
wenye hasira kali kwa kuwaadhibu watu pindi wawakamatapo kwa kigezo
cha hasira kali".
"Wote tunajua kuwa rushwa ni adui wa haki,maelekezo yameshatoka kwa
watu wote wanaopenda kutoa rushwa,wataziacha familia zao".
"Pia amesema kama kuna mtu atakaetoa taarifa za uhakika,juu ya wale
wanaosumbua kibiti na amesema majibu yatapatikana ndani ya muda
mfupi,amesema hakuna safu mpya atakayokuja nayo bali polisi ni
walewale na anaamini atashirikiana nao vizuri sana kuhakikisha
usalama unaimarika".
"Kazi ya upelelezi haina muda maaalumu lakini, wananchi wasubiri majibu mazuri hasa walio raia wema,walio raia wema hawana sababu ya kukimbia na tutaenda kuzungumza nao muda si mrefu,bali waliofanya mambo maovu lazima wakimbie mapema sana".
No comments:
Post a Comment