Leo Mei 31, 2017 majira ya mchana kwa saa za hapa Tanzania
zilisambaa taarifa ambazo zilikuwa zinaeleza kifo cha aliyewahi kuwa
Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo.
Hivyo baada ya kuenea kwa habari hizo,Mwenyekiti wa Kambi rasmi ya
Upinzani Bungeni Mh “Freeman Mbowe“amekutana na Waandishi wa
Habari Dodoma ili kutoa uthibitisho huo.
Ameeleza amependa kuthibitisha kuhusu habari zinazoendelea
kusambaa za kifo cha Mzee Ndesamboro,amesema ni kweli tukio hilo
limetokea,na hivi karibuni alikuwa mjini Dodoma,ambapo baada ya
kurejea Moshi na kufanya mazungumzo na wadau kadhaa akiwemo meya wa
Arusha kwa lengo la kuweza kutoa rambirambi kwa tukio la wahanga wa
ajali ya Luck Vincent.
“Imeelezwa kuwa alipoanza kuandika check,ya rambirambi hiyo
ndipo akaanza kupoteza nguvu,ambapo walimkimbiza hospitali
wakishirikiana na wanafamilia,na baada ya mda kiasi ndipo madaktari
walikuja na kueleza kuwa mzee wetu amepoteza maisha.”
“Hakika chama kimepoteza mtu shujaa,na wa muhimu mno.hivyo kwa
kutambua mchango wake,tutawajulisha watanzania wote kupitia vyombo
vya habari tofauti na hata kwa kutumia mitandao ya kijamii ili
taarifa hii iwafikie watanzania wengi zaidi”.
No comments:
Post a Comment