Wabunge
kadhaa wajadiliwa kwa vitendo vya kudharau mamlaka ya spika wa bunge
na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,baadhi yao ni kama
Freeman Mbowe,Halima Mdee.
Ambao
walipelekwa kwenye kamati ya haki,maadili na madaraka ya bunge,na
baada ya kamati hyo ya bunge kupitia vizuri shauri mashauri yao wameazimia
kumsamehe, na kumshauri kuwa mfano kwa wabunge wengine,kwakuwa yeye
ndiye kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani hivyo itapendeza akiwa
mfuata utaratibu wa kawaida wa bunge kwa kuzingatia miongozo
inayoliendesha bunge hilo.
Lakini
kwa upande wa Halima mdee,ameonekana kuonesha kitendo cha kudharau
mamlaka ya spika na kutoka maneno yasiyokuwa ya kiungwana,hivyo
kamati baada ya kukaa na kumtia hatiani inapendekeza kuwa,kutokana na
kujirudia kwa tukio hilo hivyo mh Halima Mdee asihudhurie vikao vyote
vya bunge vilivyosalia ili aweze kujifunza na kung'amua makosa yake.ndipo mh Halima Mdee alipoliomba radhi bunge na spika na kuahidi kurekebisha vitendo hivyo na mwishowe adhabu ilitenguliwa nahivyo ataendelea na vikao vya bunge kama kawaida.
haya
yameelezwa leo bungeni na makamu wa mwenyekiti wa kamati ya maadili
na madaraka ya bunge:Mh
Almasi Maige.
No comments:
Post a Comment