• DON'T MISS

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****
    RABA CLASSIC

    Saturday, 20 May 2017

    Yanga yanyakua ubingwa kimya kimya mbele ya Mbao FC,Huku Simba SC wakiiadhibu Mwadui.

    Kikosi cha Yanga ambao ndio mabingwa mara tatu mfululizo wa ligi ya Vodacom, kimeshuka dimbani dhidi ya Mbao FC kwenye mchezo wa uliopigwa pale uwanja wa CCM Kirumba jijini mwanza.
    Mchezo ambao umemalizika kwa timu ya wana jangwani Yanga kufungwa na mbao kwa goli la kujifunga kwenye dk 26 ya mchezo kupitia Andrew Vicent alipotaka kuokoa mpira langoni kwao hivyo kuwafanya Mbao FC kutoka kifua mbele ikiwa ni muendelezo wa kuwakamia mabingwa hao wa VPL.
    Yanga wamenyakua ubingwa huu wakiwa sawa kwa pointi na watani wao wa jadi Simba SC,kwa kila timu kuwa na pointi 68 kibindoni,ila ikiwa na wastani mzuri wa magoli ya kushinda.

    Matokeo ya michezo mingine ya VPL na timu zilizoshuka daraja.

    Simba 2 -1 Mwadui FC

    Majimaji 2 -1 Mbeya City

    Mtibwa 3 - 1 Toto Africans

    Ndanda 2 - 0 Jkt Ruvu.

    Azam 0 - 1 Kagera sugar.
    Timu zilizoshuka daraja.

    -Afrika Lion

    -Toto Africa

    -JKT Ruvu 

    No comments:

    Post a Comment