Klabu ya soka ya Simba ya jijini dar es salaam,imewachapa klabu ya soka ya African Lyon na katika mchezo wao uliochezwa leo tar mei 07,2017 kwa jumla ya mabao 2-1.
Simba SC imefanikiwa kufikisha jumla ya pointi 62 katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara,ikiwa imeshacheza michezo 28 hadi sasa.
kwa sasa simba ndiye anayeongoza ligi wakifuatiwa na Yanga kwenye nafasi ya pili katika msimamo huo wa ligi ambapo wao wana pointi 59 wakiwa na michezo minne mkononi.
No comments:
Post a Comment